Pata Mengi Zaidi

TECNO Mobile, iliyoanzishwa mwaka wa 2006, ni jina la simu ya hali ya juu iliyoundwa na Transsion Holdings. Kama mtoaji nambari moja Afrika wa simu za SIM kadi mbili, TECNO inaangazia kuimarisha teknolojia za ubunifu wa hali ya juu kwa masoko yanayoibuka, kutoa bidhaa zilizobinafsishwa chini ya mwongozo wa “Think Globally, Act Locally”, yaani Waza Kimataifa, Tekeleza Kitaifa.

 • TECNO Mobile Imezinduliwa katika Soko la India

  2017-01-01

  TECNO Mobile Imezinduliwa katika Soko la India

  TECNO imepanua uwepo wake barani Afrika, Mashariki ya Kati, Asia Kusini Mashariki, Asia Kusini na Amerika Kusini, na kuangazia watu zaidi ya bilioni 4.2.

 • TECNO Mobile Partnership with MCFC

  Ushirikiano na MCFC

  2016-01-01
  TECNO Mobile Partnership with MCFC

  Ushirikiano na MCFC

  TECNO ilianzisha ushirikiano wa miaka mingi na Klabu ya Kandanda ya Manchester City, kama mbia rasmi wa tableti na simu za mkononi. Ushirikiano huu unahudumu kama hatua muhimu katika mkakati wa kiulimwengu wa TECNO na unaonyesha hamu yake ya kutengeneza bidhaa yenye ushawishi mkubwa zaidi na inayopendelewa zaidi katika masoko yanayoibuka. Kushirikiana na klabu yenye mafanikio na inayojulikana vyema kama Manchester City, TECNO ina nafasi bora zaidi kuunganisha na mashabiki na watumiaji kote ulimwenguni, kuleta upya miundo yake ya hivi sasa zaidi na kuwapa huduma bora zaidi ya vifaa vya mkononi. 

 • TECNO Mobile Success in North Africa, and Expansion into South America and Southeast Asia

  Mafanikio katika Afrika Kaskazini, na Upanuzi hadi ndani ya Amerika Kusini na Asia Kusini Mashariki

  2016-01-01

  Mafanikio katika Afrika Kaskazini, na Upanuzi hadi ndani ya Amerika Kusini na Asia Kusini Mashariki

  Baada ya ukuaji wa haraka wa muongo mmoja, TECNO ilipata hadi mgao wa soko wa 40% katika nchi kuu za Afrika, na kukita mizizi kama mwanachama wa kimataifa wa vifaa na huduma za mawasiliano. Mafanikio haya yamechangiwa na mkakati thabiti na usimamizi dhubuti, unaojumuisha vituo 5 vya utengenezaji, vituo 5 vya uuzaji, mtandao wa mauzo wa takriban nchi na kanda 50, na mtandao wa baada ya mauzo wa zaidi ya vituo 1000 vya huduma na viwanda 4 vya ukarabati. Mwaka huu pia umeshuhudia mafanikio ya kimkakati ya TECNO ya kupanuka hadi ndani ya Afrika Kaskazini, Amerika Kusini, India, Mashariki ya Kati na kupenyeza katika soko la kiulimwengu. 

 • Sales Volume Rose to No.1 in Major African Markets - TECNO Mobile

  Mauzo Yapanda hadi Nafasi ya 1 katika Masoko Makuu ya Afrika

  2015-01-01
  Sales Volume Rose to No.1 in Major African Markets - TECNO Mobile

  Mauzo Yapanda hadi Nafasi ya 1 katika Masoko Makuu ya Afrika

  Mauzo ya TECNO yalipanda hadi nafasi ya 1 katika masoko makuu ya Afrika mwaka wa 2015
  Katika jitihada kuu na uelewa mkuu wa mahitaji ya watumiaji, TECNO imepiga hatua kubwa katika R & D, muundo, utengenezaji, mauzo na huduma. Hivyo, iliimarisha ushirikiano na kampuni kuu zaidi katika nyanja zao. Vipengele vyote viliungana kuendesha ukuaji wa bidhaa na mgawo wa soko. TECNO Phantom Z ilipewa tuzo ya “Simu janja Bora Zaidi ya mwaka” katika Tuzo za Ghana Telecom. Huku ikifanikisha biashara yake, TECNO inachukua jukumu amilifu katika kuchangia jamii. Ilishirikiana na mashirika ya ndani ya msaada ili kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa ndani na kutoa misaada ili kusaidia miradi ya kiserikali.

 • TECNO Mobile Breakthrough in Smartphones

  Hatua Kubwa katika Simu janja

  2014-01-01
  TECNO Mobile Breakthrough in Smartphones

  Hatua Kubwa katika Simu janja

  Huku ikidumisha ukuaji thabiti katika soko la simu za kawaida, kampuni ilifanikiwa katika soko la simu janja, ilifanya hatua kubwa katika kutambulika kote ulimwenguni na kufungua zaidi ya maduka 860 katika Mataifa ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara. Muda huo huo, ilipanuka nje ya Mataifa ya Afrika - Kusini mwa Jangwa la Sahara na iko tayari kukuza soko la Misri. TECNO ilitajwa kuwa “Bidhaa yenye dira zaidi” na “Bidhaa Inayoinuka Zaidi” katika Tuzo za Bidhaa Bora nchini Ghana. Kifaa chake kikuu Phantom A+ kilitunzwa tuzo la "Simu janja Maarufu Zaidi za Mwaka” na Mobile World nchini Ghana. TECNO pia ilitajwa katika “Bidhaa 20 Bora Zinazovutia Zaidi barani Afrika” na jarida la African Business, jaridi la biashara lenye ushawishi mkubwa zaidi barani. Pia katika mwaka huu, TECNO ilituzwa Tuzo la Taji la Kimataifa la Ubora katika Kipengele cha Dhahabu mjini London.

 • Introducing Smartphones -TECNO Mobile

  Inatambulisha Simu janja

  2012-01-01
  Introducing Smartphones -TECNO Mobile

  Inatambulisha Simu janja

  Katika kukabiliana na maendeleo makubwa ya kiteknolojia na mahitaji yanayoongezeka ya watumiaji, TECNO ilizindua simu janja yake ya kwanza T1 na kuanzisha mawasiliano ya uuzaji wa simu hii mwaka wa 2012. Kando na kuunda simu janja za ubora wa juu na kuwaletea watumiaji burudani kabambe, TECNO ilianzisha duka lake nchini Naijeria, ambapo ilionyesha ubunifu wa hivi sasa zaidi na kutoa huduma za hali ya juu kwa watumiaji. TECNO Ghana ilitajwa kuwa “Kampuni Bora Zaidi ya Simu kwa Mwaka” katika Tuzo za Ghana Telecom, ambazo zimebuniwa kupongeza ukuaji na mafanikio ya soko la Teknolojia ya Taarifa Mawasiliano na kuangazia waliofanya vyema zaidi na wenye ubunifu zaidi ndani ya sekta. Mauzo ya kimwaka ya TECNO yalifikia takriban milioni 20 mwaka wa 2012.

 • No. 1 Mobile Brand of Dual-SIM Phones of TECNO Mobile

  Bidhaa Na. 1 ya Simu za SIM Kadi Mbili

  2011-01-01
  No. 1 Mobile Brand of Dual-SIM Phones of TECNO Mobile

  Bidhaa Na. 1 ya Simu za SIM Kadi Mbili

  TECNO ilikuwa mtengenezaji Na. 1 wa simu za SIM kadi mbili katika masoko makuu Afrika ambapo ofisi za ndani zilikuwa zimewekwa. Ilitajwa kuwa “Bidhaa Inayoaminiwa Zaidi na Wateja katika Mwaka wa 2011/2012” katika Tuzo za Huduma za Wateja nchini Ghana kama sehemu ya Wiki ya Huduma za Wateja nchini Ghana, tukio la kote ulimwenguni linaloadhimishwa katika wiki ya kwanza kamili ya mwezi Oktoba kila mwaka wakati mashirika na asasi zinazowahudumia wateja kote ulimwenguni zinapotambua umuhimu wa Huduma Bora za Wateja. Hivyo, TECNO ikabuni kauli ya bidhaa ya “Experience More”, yaani Pata Huduma Bora Zaidi, na kuhamasisha tafiti katika teknolojia za rununu na vifaa vinavyoangazia burudani, na kuwaletea wateja huduma ya hali ya juu ya burudani.

 • TECNO Mobile Focus on Africa

  Kuangazia Afrika

  2008-01-01
  TECNO Mobile Focus on Africa

  Kuangazia Afrika

  Mwaka wa 2008 umeshuhudia badiliko la mkakati wa TECNO katika kuangazia soko la Afrika na kuashiria mwanzo wa kutambulisha bidhaa ya TECNO. TECNO ilipanga na kuunda mfumo wa usimamizi wa ughaibuni ili kusimamia masoko makuu barani Afrika Magharibi na Afrika Mashariki, katika juhudi ya kutoa bidhaa zilizobinafsishwa kwa mahitaji ya ndani na huduma bora zaidi kwa watumiaji wa nchini. Ikihamasishwa na michango ya watumiaji, TECNO iliunda simu yake ya kwanza ya SIM kadi nne “4 Runner”, ambayo ilipata umaarufu na kufanya vyema barani Afrika.

 • 1st Factory Setup of TECNO Mobile

  Kiwanda cha 1 Kujengwa

  2007-01-01
  1st Factory Setup of TECNO Mobile

  Kiwanda cha 1 Kujengwa

  Kiwanda cha kwanza kilianzishwa mjini Shenzen, Uchina mwaka wa 2007. Uwezo wa utengenezaji wa kimwaka wa kiwanda hiki ulifikia simu za mkononi milioni 3. Kwa kutumia teknolojia za hali ya juu zaidi na kuwaajiri wafanyikazi wenye utaalamu zaidi, TECNO ilifanikisha matokeo mazuri ya kibiashara.

 • Establishment of TECNO Mobile

  Kuanzishwa

  2006-01-01
  Establishment of TECNO Mobile

  Kuanzishwa

  TECNO Mobile, iliyoanzishwa mwaka wa 2006, mjini Hong Kong, ndiyo bidhaa ya simu ya mkononi ya kwanza ya Transsion Holdings,kampuni ta teknolojia za hali ya juu inayotangamanisha utafiti, ubunifu, utengenezaji, mauzo na huduma za bidhaa za mawasiliano. TECNO inajitahidi kutoa ufumbuzi unaoridhisha wa mawasiliano ya kwa watumiaji.

TECNO ilitangaza ushirikiano wa miaka mingi na Klabu ya Kandanda ya Manchester City mnamo Novemba 2016. Kama Mbia Rasmi wa Tableti na Simu za Mkononi wa Klabu ya Kandanda ya Manchester City, TECNO Mobile itashirikiana na Klabu hii ili kukuza matangazo yake ya uuzaji kote ulimwenguni. , na kuunganisha na mashabiki na wateja ili kuwapa huduma bora zaidi.

Habari za Hivi Sasa

Pata maelezo zaidi