Sera ya Faragha

Sera ya Faragha

Sera ya Faragha

Sera hii ya Faragha inaeleza jinsi Tecno, pamoja na matawi na washirika wake (“Tecno,” “sisi,” “yetu,” “zetu”) wanavyokusanya, kusindika, kutumia, kushiriki, kufichua, kuhifadhi, na kulinda taarifa yako. Ni muhimu kwamba usome na uelewe Sera hii ya Faragha kwa sababu unatumia huduma zetu, itachukuliwa kwamba umekubali matendo yaliyotajwa katika Sera ya Faragha. Ikiwa hauridhiki na matendo yaliyoelezwa katika Sera hii ya Faragha, haupaswi kutumia huduma zetu.


I. Ukusanyaji Taarifa

1. Taarifa ya Kibinafsi Uliyoitoa Moja kwa Moja

Unapotumia bidhaa na huduma zetu zinazopatikana kwenye au kupitia tovuti yetu rasmi (“Tovuti”) au unaposajili akaunti nasi, huenda ukatoa taarifa fulani inayokutambulisha kibinafsi inayokuhusu wewe ambayo inaweza kutumiwa ikiwa peke yake au pamoja na taarifa nyingine ili kumtambua mtu binafsi, kuwasiliana naye, ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, jina lako, anwani ya barua pepe, anwani ya barua, Kitambulisho cha mtumiaji, nenosiri, nambari ya simu, nambari ya faksi, mapendeleo ya mawasiliano, tarehe ya kuzaliwa, anwani, picha, video na demografia (jinsia, umri, kazi, jina la kampuni au shirika, mapendeleo ya lugha, mji, nchi, msimbo wa zip, msimbo wa eneo, eneo la saa, n.k.). Ukinunua huduma au bidhaa kutoka kwetu, pia huenda tukachukua nambari ya ununuzi, historia ya muamala, tarehe/saa za kununua, taarifa ya bidhaa na kumbukumbu za hitilafu, historia ya kurejeshewa fedha, taarifa ya kadi ya mkopo au mjazo au taarifa nyingine ya malipo, taarifa ya akaunti ya benki, anwani haswa au kadiri la anwani ya kijiografia ya bidhaa yako, taarifa ya kurejeshewa fedha na ukarabati inayohusiana na bidhaa au maoni yako kuhusiana na bidhaa au huduma, na taarifa nyingine zisizo za hadharani. Huenda tukahifadhi taarifa yoyote unayotupatia pamoja na taarifa zilizokusanywa kutoka kwa vyanzo vingine, ikijumuisha akaunti za kijamii ambazo unachagua kuhusishswa na utumizi wako wa huduma, au pamoja na taarifa tunayopokea kutoka kwa kampuni nyingine.

2. Taarifa Isiyo ya Kibinafsi

Pia tunaweza kukusanya taarifa fulani isiyo ya kibinafsi, inayojumuisha, lakini sio tu, muundo wa kifaa, vitambulisho vya kifaa (k.m. IMEI, MEID, nambari tambulishi, CID, MID na Nambari ya Utambulisho ya MCC au Kitambulisho cha kadi ya SIM), anwani ya MAC, tarehe uliyoamilisha kifaa chako, aina na matoleo ya mfumo wako msingi unaoendesha, maudhui unayotazama au kutumia na kumbukumbu zenye mida za ubadilishanaji data, anwani ya Itifaki ya Itaneti (IP), takwimu za utumizi, takwimu za utendakazi, historia ya kuvinjari na urambazaji, anwani umla ya kijiografia, mida ya ufikiaji, aina ya kisakuzi, tovuti uliyotembelea kabla ya na baada ya kutembelea Tovuti, jina la tovuti ya mtoa huduma ya intaneti kwako, programu unazopakua na kusakinisha, mtoa huduma ya simu kwako, utangamano wako na maudhui na programu kupitia bidhaa na huduma zetu. Pia tunaweza kukusanya taarufa inayokuhusu wewe kutoka kwa vyanzo vinavyopatikana hadharani au kibiashara (kama inavyoruhusiwa na sheria), taarifa inayokuhusu wewe kutoka kwa vyombo vingine vya huduma za mitandao ya kijmii unapochagua kuunganisha na huduma hizo au tunapotumia vyombo vingine vinayotoa huduma za matangazo katika huduma zetu. Ili kuwasilisha matangazo haya, vyombo vingine vinachukua otomatiki taarifa fulani inayokuhusu wewe na vifaa vyako na utumizi wako wa Tovuti, ikijumuisha lakini sio tu taarifa iliyotajwa hapa juu.

Kwa madhumuni ya Sera hii ya Faragha, hapa unakubali kwamba vyombo hivyo vinginekama ilivyotajwa hapa juu vinaweza kushiriki taarifa iliyokusanywa hapo juu pamoja na Tecno, jambo ambalo halitachukuliwa kuwa ukiukaji wa makubaliano ya faragha, ikiwa yapo, kati yako na vyombo hivyo. Aidha, kwa kukusanya taarifa yako kutoka kwa vyombo hivyo vingine kwa njia iliyotajwa hapa juu, Tecno haitachukuliwa kukubali kufungwa na makubaliano yoyote ya faragha kati yako na vyombo vingine kuhusiana na taarifa yako.

II. Usindikaji na Utumizi wa Taarifa

Huenda tukasibdika au kutumia taarifa yako ili kupanga a kusindika ununuzi, ikijumuisha uthibitishaji, ankara, arifa za kiusalama na ujumbu wa usaidizi; kukutumia ilani kuhusiana na miamala yako, kama vile mawasiliano kuhusu ununuzi na mabadiliko kwenye sheria, masharti, na sera zetu; ili kutoa na kuwasilisha bidhaa na huduma unazonunua; ili kusajili, kuamilisha, kuthibitisha na kusasisha bidhaa na huduma zako; ili kujibu maswali na maoni yako; ili kutoa udumishaji na kusuluhisha matatizo kwenye Tovuti, bidhaa na huduma zako; kukupa mapasho kuhusu matangazo ya hivi sasa zaidi ya bidhaa za Tecno, sasisho za programu, na matukio yanayoibuka; kutusaidia kutengeneza, kuendesha, na kuimarisha bidhaa, huduma, tovuti, uuzaji na uhusiano wetu na wateja; ili kuchunguza ulaghai, shughuli yoyote ambao haijaidhinishwa au si halali; ili kutumia kwa madhumuni ya ndani kama vile ukaguzi, uchanganuzi data, ili kuwasiliana nawe kuhusu promosheni na tuzo kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na Tecno (unaweza kuondoa usajili wako wa kuokea barua pepe za promosheni kwa kubonyez kiungo cha kuondoa usajili kilicho ndani ya barua pepe hiyo); ili kutoa maudhui yaliyobinafsishwa na kufanya mapendekezo kulingana na shughuli zako kwenye huduma zetu; ili kutoa matangazo yaliyobinafsishwa; ili kuomba maoni yako kuhusu bidhaa na huduma zetu na kufanya tafiti za wateja.

III. Teknolojia

Tunatumia aina tofauti ya teknolojia ili kukusanya taarifa unapotumia huduma na bidhaa zetu au unapotembelea Tovuti yetu, inayojumuisha kuki, nguzo za wavuti na tecknolojia nyingine, kama vile Local Shared Objects (LSOs, pia zinaitwa “Flash Cookies”). Kuki ni faili ndogo zinazohifadhi taarifa kwenye kompyuta yako, simu yako ya mkononi au kifaa chako kingine. Zinaweza kukumbuka data na mipangilio yako, kama vile ukubwa wa mwabdiko, na mapendeleo mengine, ambayo yanaweza kutusaidia kuchanganua utangamano wako na tovuti yetu kwa ajili ya kukuza huduma zetu na huduma bora kwako. Kando na hayo, haya yana manufaa kwetu katika kuelewa ni sehemu gani ya tovuti yetu na ni vipengele gani ni maarufu zaidi. Pia tunatumia taarifa iliyokusanywa na kuki katika kulenga matangazo yetu. Nguzo za wavuti ni picha za kielektoniki zilizounganiushwa na maudhui ya mtandaoni, video, na barua pepe, na zinaweza kuwezesha seva kusoma aina fulani ya taarifa kwenye kompyuta yako au simu yako ya mkononi na kuhesabu mara uliyotembelea tovuti. Tunatumia kuki kuhifadhi mapendeleo yako kulingana na unachotembelea kwenye Tovuti ili kubinafsisha matembezi yako.

Unapotembelea Tovuti, unaweza kubadilisha mipangilio ya kisakuzi chako ili kufuta au kuzuia kuki kutohifadhiwa kwenye kompyuta yako au simu yako ya mkononi kwa kutazama menyu ya “usaidizi” kwenye kisakuzi chako ili kukubali kuki zote, kukataa kuki zote, au kukuarifu wakati kuki inapotumwa. Hata hivyo, baadhi ya huduma huenda zimeundwa kufanya kazi zikitumia kuki, na kulemaza kuki huenda kukaathiri uwezo wako wa kutumia huduma hizo, au sehemu fulani ya huduma hizo.

Kwa kufikia na kutumia huduma zetu, unatoa ridhaa ya kuhifadhiwa kwa kuki, teknolojia nyingine zinazohifadhiwa kwenye kifaa, nguzo na taarifa nyingine kwenye kifaa chako. Pia unatoa ridhaa ya sisi na vyombo vingine vilivyotajwa hapo juu kufikia kuki, teknolojia za hifadhi ya ndani, nguzo na taarifa hizo.

IV. Ufichuaji kwa Vyombo Vingine

Huenda tukashiriki taarifa yako ya kibinafsi na washiriki wetu, wabia wetu wa biashara au kampuni ambazo zinatoa huduma kama za kusindika taarifa, kutoa mikopo, kutimiza ununuzi wa wateja, kuwasilisha bidhaa kwako, kusimamia na kuimarisha data za wateja, kutoa huduma kwa wateja, kutathmini mapendeleo yako kwa bidhaa na huduma zetu, na kuendesha tafiti za wateja au za kuridhika kwa wateja. Pia tunaweza kushiriki taarifa yako tunapoghitajika na sheria, mchakato wa kisheria, kesi, na maombi kutoka kwa mamlaka za umma au za serikali ndani na nje ya nchi yako unakoishi ili kufichua taarifa yako ya kibinafsi. Pia tunaweza kuvumbua taariafa yako tuking’amua kwamba ufichuaji huo niwa muhimu kaika kutekeleza sheria na masharti yetu au ili kulinga operesheni zetu na watumiaji wetu. Aidha, katika tukio la mipango mipya, kuungana na wengine, kununuliwa, au katika tukio la kufirisika huenda tunafichua taarifa yoyote na zote za kibinafsi zilizotolewa kwa vyombo vingine husika. Pia tutafichua taarifa yako kwa vyombo vingine kwa madhumuni yako huru ya matangano au kibiashara bila ridhaa yako.

Kwa ajili ya Sera hii ya Faragha, unaachilia haki yako ya kuibua madai dhidi ya Tecno, ikijumuisha kampuni zake tanzu na washirika wake, kwa kushiriki, kufichua na kuvumbua taarifa yako kulikoelezewa hapo juu.

V. Kuhifadhi Taarifa

Tutalinda taarifa zako zote za kibinafsi kulingana na Sera hii ya Faragha. Taarifa yako ya kibinafsi. huenda ikahifadhiwa kwa kipindi kinachohitajika ili kutimiza madhumuni yaliyotajwa katika Sera hii ya Faragha, au kwa kipindi kinachohitajika au kuruhusiwa na sheria na kanuni husika.

VI. Huduma Zinazotegemea Anwani

Tunapotoa huduma zinazotegemea anwani kwenye bidhaa za Tecno, huenda tukakusanya na kutumia data ya muda halisi ya anwani za kijiografia, ambazo zinaweza kupatikana kwenye taarifa za Mfumo wa Eneo wa Kiulimwengu (GPS), eneo tete la Wi-Fi, Bluetooth, au nambari ya utambulisho ya mnara wa mitambo wa mtandao wa mtoa huduma ya simu kwako. Unaweza kuwasha, au kuzima taarifa zako za GPS kwa kwenda kwenye mipangilio ya GPS kwenye bidhaa, lakini huenda ukawa hauna haki ya kudhibiti Wi-Fi na nambari za utambulisho za mnara wa mitambo wa mtandao wa mtoa huduma ya simu kwako kwani hili linategemea sera ya mtoa huduma ya simu kwako.

VII. Ulindaji Taarifa ya Kibinafsi

Tunajaribu kulinda taarifa ya kibinafsi kwa kuchukua hatua mwafaka za kiufundi na kimpangilio dhidi ya ufikiaji au utumizi amabo haujaidhinishwa wa taarifa yako ya kibinafsi. Hata ingawa tutachukua hatua za busara ili kutumia na kuimarisha ulinzi wetu, hakuna mfumo wala teknolojia ambayo ni salama kikamilifu. Hata hivyo, tafadhali kumbuka kwamba hata ingawa tutachukua hatua za busara ili kulinda taarifa yako ya kibinafsi, hakuna tovuti, wasilisho la Intaneti, mfumo wa kompyuta au muunganisho wa pasi waya ni salama kikamilifu. Kando na hayo, hatuwajibikii usalama wa programu na huduma zozote za chombo kingine huru au data ambayo inaweza kukusanywa kukuhusu na programu na huduma hizo za chombo kingine. Tafadhali viulize vyombo hivyo vingine jinsi vinavyoweka data yako salama.

Tafadhali kumbuka kwamba taarifa yako ya kibinafsi unayochagua kushiriki katika baadshi ya matumiko huenda ikafikiwa na watumiaji wengine na inaweza kusomwa, kukusanywa, kunakiliwa, kuchapishwa au kutumiwa na watumiaji hao. Unapaswa kuwajibikia kibinafsi taarifa ya kibinafsi unayochagua kushiriki au kuwasilisha katika matukio hayo. Unafaa kuwa mwangalifu unapoamua ni taarifa gani ya kibinafsi unataka kushiriki au kuwasilisha.

VIII. Ulindaji Watoto

Tunathamini sana ulinzi wa taarifa ya kibinafsi ya watoto. Ikiwa wewe ni mtoto, unafaa kumuomba mlezi wako kusoma na kuelewa Sera hii ya fragha kwa unangalifu. Unapaswa kuthibitisha kwamba unatumia huduma zetu na/au unatupatia taarifa baada ya kupokea ridhaa ya awali ya mlezi wako. Kwa madhumuni ya Sera hii ya Faragha, mtoto hapa itamaanisha kama ilivyobainishwa na sheria katika nchi ambako wanaishi kwa kawaida.

IX. Mabadiliko kwenye Sera ya Faragha

Sera hii inaweza kubadilishwa mara kwa mara. Tunapobadilisha sera hii, kutakuwa au HAKUTAKUWA na ilani iliyochapishwa kwenye Tovuti an Sera mpya itaaza kutumika baada ya kuchapishwa kwenye Tovuti. Unafaa kukagua Sera hii kama imesasishwa upya mara kwa mara. Inaporuhusiwa na sheria, mabadiliko yoyote muhimu katika jinsi ambavyo tunakusanya, kusindika, kutumia, kushiriki, kufichua, kuhifadhi na kulinda taarifa inayotambulisha kibinafsi yatatumika tu kwa taarifa iliyokusanywa baada ya Sera iliyorekebishwa kuchapishwa.

X. Sheria Husika na Usuluhishaji Migogoro

Mgogoro, dai, tofauti au utata wowote mwingine unaoibuka kutokana au kuhusiana na Sera hii ya Faragha utatawaliwa, utakuwa chini na utatafsiriwa kulingana na sheria za Hong Kong, bila kuzingatia matukio ya ukinzani wa sheria husika. Mgogoro au tofauti yoyote kuhusiana na Sera hii ya Faragha ambayo haiwezi kutatuliwa kikamilifu itatumwa na kusuluhishwa kikamilifu kwa suluhu inayotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Suluhu cha Hong Kong (HKIAC) chini ya Sheria za Suluhu Inayotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Suluhu cha Hong Kong zinazotumika wakati Ilani ya Suluhu inapowasilishwa. Usuluhishaji utafanyikia Hong Kong. Lugha ya usuluhishaji itakuwa Kiingereza. Suluhu itakayotolewa itakuwa ya mwisho na itafuatwa na wahusika walio na mgogoro.

XI. Maswali na Mawasiliano

Ikiwa una maswali au wasi wasi zozote kuhusiana na Sera yetu ya Faragha au ikiwa ungependa kuwasilisha lalamishi la ukiukaji wa sheria za nchini za faragha, unaweza kuwasiliana nasi kwa kutumia (Email).

Hakimiliki © 2017 Tecno Inc. Haki zote zimehifadhiwa.