Sheria za Utumizi za TECNO

Sheria za Utumizi za TECNO

Sheria za Utumizi za TECNO

Karibu kwenye TECNO! Utumizi wako wa tovuti hii unajumuisha ukubali wako wa kuambatana na Sheria za utumizi.


I. Ukubali wa Sheria

Sheria hizi za utumizi (“Sheria”) yanatumika kati yako na Tecno Inc., ikijumuisha kampuni zake tanzu na washirika wake (“Tecno”, “sisi”, “yetu” au “zetu”), kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria, haswa kuhusiana na ufikiaji au utumizi wa tovuti rasmi ilito kwenye (“Tovuti”). Tunakukumbusha kwamba kabla ya kufikia au kutumia Tovuti, tafadhali soma kwa uangalifu na usome Masharti haya. Kwa kubonyeza kitufu cha kukubali au kwa kutumia Tovuti kwa namna yoyote, unaonyesha ukubali wako wa kuambatana kisheria na Sheria hizi. Ikiwa haukubaliani na sheria hizi, hautafikia wala kutumia Tovuti.

Huenda ukawa chini ya sheria au masharti ya ziada ambayo yameunganishwa katika Sheria hizi kwa kurejelewa unapotumia vipengele fulani vya Tovuti au nyenzo za ziada kutoka kwa Tovuti, ambayo yanakuhitaji kuambatana na sheria na masharti haya ya ziada. Ukikosa kukubali sheria na masharti haya ya ziada, hautatumia vipengele hivi vya ziada vya Tovuti.

II. Urekebishaji wa Sheria

Tunahifadhi haki ya kusasisha, kurekebisha, kujaza, kufuta, kuahirisha au kufutilia mbali Sheria hizi na ufikiaji wako kwenye Tovuti au sehemu yoyote yake (“sasisho”), wakati wowote, bila ilani, na unapaswa kukagua sasisho hizi mara kwa mara. Sasisho hizi zitaanza kutumika baada ya kuchapishwa, na ukiendelea kutumia Tovuti baada ya kuchapishwa kwa sasisho hizi kunamaanisha unakubali kisheria toleo jipya a Sheria.

III. Maudhui

Taarifa zote zinazopatikana kwenye Tovuti, ikijumuisha lakini sio tu vificho vya kompyuta, grafu, maandishi, violesura vya mtumiaji, violesura vya kuonekana, picha, faili za sauti, video, failia za muziki, picha za usanii, alama, nembo (“Maudhui”) zitakuwa mali ya Tecno na wanao ipa leseni, ikijumuisha mwonekano, hisia, muundo, muonyeshano, ujenzi, uchaguzi, na mpangilio wa Maudhui. Tecno na wanao ipa leseni watamiliki haki zote za kisheria, umiliki na manufaa ya Maudhui, ambazo ziko chini ya ulinzi wa sheria husika za hakimiliki na alama za biashara, na chini ya sheria na kanuni za mali ya kiakili na ushindani usio wa haki.

IV. Kipimo cha Utumizi wa Tovuti

Tecno inakupa leseni ya kibinafsi isiyo ya kipkee, isiyoweza kuhamishwa, isiyoweza kubatilishwa, na yenye kipimo ya kufikia na kutumia Tovuti na Maudhui kwa madhumuni ya kibinafsi pekee na isiyo ya kibiashara, mradi tu uzingatie Sheria hizi. Hautanakili, kuzalisha tena, kusambaza tena, kuchapisha tena, kuuza, kupeperusha, kupakia, kuchapisha, kuonyeshana hadharani, kusimba, kutafsiri, kuwasilisha au kuweka kwenye fremu taarifa yoyote iliyojumuishwa kwenye Tovuti pamoja na viungo bila kwanza kupata ruhusa kwa maandishi kutoka kwa Tecno au wanao ipa leseni. Unakubali kutowekea mfumo wa Tovuti uzito mwingi kupindukio, au mifumo yoyote iliyounganishwa na Tovuti na kutosambaza sehemu yoyote inayopatikana kwenye Tovuti kwa makundi mapya, orodha mpya za barua pepe, au jukwaa za mapasho. Unakubali kwamba hauna haki ya kurekebisha, kuhariri, kubadilisha au kuongeza sehemu yoyote ya Maudhui kwa namna yoyote.

Aidha, unakubali kutumia Tovuti kuchapisha, kutuma na kupokea tu ujumbe na nyenzo ambazo ni mwafaka na zinahusiana na Tovuti. Ni lazima usitumie vibaya Tovuti kwa kuweka virusi, trojani, au nyenzo nyingine ukifahamu ambazo zinaweza kuleta madhara ya kiufundi. Unakubali kutojaribu kufikia bila idhini sehemu yoyote ya Tovuti, au kukiuka hatua za idhini za seva, kompyuta, au hifadhidata zozote zilizounganishwa na Tovuti kwa kudukua au kwa njia nyongine yoyote isiyohalali. Unakubali kutotumia sehemu yoyote ya Tovuti kwa dhumuni lolote ambalo si halali au limepigwa marufuju na Sheria hiz, au kuchangia shughuli yoyote isiyo halali. Leseni iliyo na kipimo itabatilishwa kiotomatiki ukikiuka yoyote ya Sheria hizi, bila ilani. Baada ya leseni kubatilishwa, unakubali kuharibu mara moja nyenzo zozoe ulizochapa au kupakua. Kando na hayo, Tecno itaripoti ukiukaji huo kwa mamlaka husika za kisheria na Tecno itashirikiana na mamlaka hizo kwa kufichua jina lako na taarifa nyingine muhimu uliyotoa.

V. Usahihi wa Taarifa

Hata ingawa Tovuti ina lengo la kutoa huduma na bidhaa za hivi sasa zaidi, kamili, na sahihi za Tecno, baadhi ya taarifa amabzo si sahihi, hitilafu za uandishi huenda zikajumuishwa katika Maudhui, amabzo zina athari mbaya kwenye ubora wa Maudhui. Unakubali kutotegemea Taarifa yoyote iliyo kwenye Tovuti hii kwa sababu imtolewa kwa matumizi yako pekee, na unakubali kwamba Tecno haiwajibiki kwa hitilafu zozote katika Maudhui, iwe zimetolewa na Tecno au chombo kingine. Tecno haihakikishii usahihi au ukamilifu wa Taarifa yoyote katika Maudhui. Hata hivyo, Tecno inaweza kubadilisha Maudhui au bidhaa zinazopatikana kwenye Tovuti wakati wowote bila ilani.

VI. Viungo vya Chombo Kingine

Viungo vinavyoelekeza kwenye tovuti au rasilimali za vyombo vingine (“Tovuti Zilizounganishwa”) huenda vikajumuishwa katika Tovuti; hata hivyo, Tecno haina udhibiti wa Tovuti hizi Zilizounganishwa na haichuki dhima kwa taarifa, matangazo, bidhaa au nyenzo nyingine zozote zilizo au zinazopatikana kwenye Tovuti hizo Zilizounganishwa. Aidha, Tovuti Zilizounganishwa zinatolewa to kwa utumizi wa wateja, jambo ambalo halimaanishi kwamba Tecno inaunga mkono Tovuti Zilizounganishwa au nyenzo zilziorejelewa pale ndani au zinazohusiana na waendeshaji wake. Katika tukio la kufikia Tovuti Iliyounganishwa au kutumia nyenzo zinazotolewa kwenye au kupitia Tovuti Zilizounganishwa, unapaswa kuhakikisha unafanya uamuzi wako huru kuhusiana na utangamano wako na Tovuti Zilizounganishwa. Unakubali kwamba madai yoyote unayoweza kuwa nayo kuhusiana na nyenzo za vyombo vingine au Tovuti Zilizounganishwa yatakuwa dhidi ya vyombo vingine husika na sio dhidi ya Tecno.

VII. Akaunti, Nenosiri na Usalama

Kwa dhumuni la kufikia au kutumia vipengele fulaji kwenye au kupitia Tovuti Zilizounganishwa, huenda ukahitajika kusajili akaunti ukitumia jina a mtumiaji na nenosiri. Ni wajibu wako kuipa Tecno taarifa a sasa, kamili na ya kweli na kudumisha faragha ya taarifa iliyorejelewa katika akaunti yako. Unafaa kuwajibika kikamilifu kwa shughuli yoyote na zote zinazofanyika chini ya akaunti yako kwa ajili ya kukosa kuweka taarifa yao faraghani ikijumuisha ada zinazoweza kutokea chini ya akaunti yako, iwe ni wewe umefanya shughuli hizo au ni mtu mwingine. Aidha, unakubali kuiarifu Teco mara moja akaunti na nenosiri lako zikipotea, zikiibiwa, zikifichuliwa kwa mtu mwingine bila idhini, au katika tukio la tishio lingine la usalama wa akaunti yako. Hauruhusiwi kutumia akaunti ya mtu mwingine wakati wowote isipokuwa uwe umepewa ruhusa ya moja kwa moja na mmiliki akaunti hiyo. Vinginevyo, watumiaji ambao hawajaidhinishwa wanaweza kufunguliwa mashtaka kwa dhima za kisheria.

VIII. Akaunti, Nenosiri na Usalama

Kwa dhumuni la kufikia au kutumia vipengele fulaji kwenye au kupitia Tovuti Zilizounganishwa, huenda ukahitajika kusajili akaunti ukitumia jina a mtumiaji na nenosiri. Ni wajibu wako kuipa Tecno taarifa a sasa, kamili na ya kweli na kudumisha faragha ya taarifa iliyorejelewa katika akaunti yako. Unafaa kuwajibika kikamilifu kwa shughuli yoyote na zote zinazofanyika chini ya akaunti yako kwa ajili ya kukosa kuweka taarifa yao faraghani ikijumuisha ada zinazoweza kutokea chini ya akaunti yako, iwe ni wewe umefanya shughuli hizo au ni mtu mwingine. Aidha, unakubali kuiarifu Teco mara moja akaunti na nenosiri lako zikipotea, zikiibiwa, zikifichuliwa kwa mtu mwingine bila idhini, au katika tukio la tishio lingine la usalama wa akaunti yako. Hauruhusiwi kutumia akaunti ya mtu mwingine wakati wowote isipokuwa uwe umepewa ruhusa ya moja kwa moja na mmiliki akaunti hiyo. Vinginevyo, watumiaji ambao hawajaidhinishwa wanaweza kufunguliwa mashtaka kwa dhima za kisheria.

IX. Uwasilishaji wa Mtumiaji

Tovuti imekusudiwa watu wazima, na pia watoto ambao wanathibitisha kwamba wana ruhusa ya walezi waoya kuwasilisha kwa kuipa Tecno taarifa yoyote kuwahusu, ikijumuisga majina yao, anwani zao, nambari zao za simu, au anwani zao za barua pepe (moja kwa oja, au kwenye jukwaa la mapasho ya tovuti, blogi, n.k.). Kwa madhumuni ya Sheria hizi, wakati wa uwasilishaji huo wa taarifa, mtu mzima na mtoto hapa itamaanisha kama ilivyobainishwa na sheria katika nchi ambako wanaishi kwa kawaida.

Kuhusiana na taarifa zote zilizowasilishwa na watumiaji (Uwasilishaji wa Mtumiaji), Tecno haiwajibiki kwa usahihi au ukweli wa taarifa hizo. Hata hivyo, Uwasilishaji wako wa Mtumiaji hauwezi kukiuka hakimiliki, alama ya kibiashara, siri ya kibiashara, au haki nyingine zozote za mali ya kiakili za mhusika yeyote, na hauwezi kukiuka sheria yoyote, ikijumuisha lakini sio tu, sheria zinazohusu ulindaji mtumiaji, ulindaji data au ushindani usio wa haki. Kando na hayo, unakubali kwamba Uwasilishaji wako wa Mtumiaji sio wa kuharibia jina, wa chuki, kimbari, kidini, usio wa haki au unaokosea mtu yeyote binafsi au kampuni. Pia unakiri kwamba Uwasilishaji wako wa Mtumiaji hautajumuisha virusi vyovyote au prograu nyingine zinazodhuru, ikijumuisha kuweka mzigo mkubwa kwenye Tovuti. Unakubali kwamba Uwasilishaji wako wa Mtumiaji hauna matangazo yoyote ambayo hayajaidhinishwa, barua taka, au aina nyingine yoyote ya ulaghai.

X. Mali ya Kiakili

Isipokuwa iwe imebainishwa moja kwa moja katika Sheria za Utumizi, hakuna chohcote kilicho hapa kitaonekana kama kinakupa wewe au chombo kingine chochote leseni au haki yoyote, kwa mwonekano, kutajwa au vinginevyo, chini ya sheria, sharti au kanuni yoyote ikijumuisha, lakini sio tu, zile zinazohusu hakimiliki au haki nyingine za mali ya kiakili. Unakubali kwamba Maudhui na Tovuti zimelindwa na hakimiliki, alama za kibiashara, alama za huduma, au haki na sheria nyingine zozote za umiliki. Alama za kibiashara, nembo, na alama za huduma (kwa pamoja "Alama") zinazotokea kwenye Tovuti ni Alama za Tecno zilizosajiliwa na ambazo hazijasajiliwa. Utumizi wa Tovuti hii na taarifa iliyo ndani yake haimaanishi kamwe Tecno inakupa leseni au haki yoyote ya kutumia Alama zoozte zilizoonyeshwa kwenye Tovuti hii. Unapigwa marufuku kutumia Alama zilizoonyeshwa kwenye Tovuti au maudhui mengine yoyote ayliyo kwenye Tovuti, isipokuwa iwe imebainishwa katika ilani za kisheria.

Tovuti hii ina maeneo ya kutangamana ambayo yanajumuisha, lakini sio tu, jukwaa lolote la mapasho, jukwaa za majadiliano, sehemu za maoni, na vipengele vya maswali na majibu ("Maeneo ya Utangamano"). Unaipa Tecno leseni isiyoweza kubatilishwa, isiyo ya kipekee, bila ada, ya milele, ya kote ulimwenguni ya kutumia, kupeana idhini ya kutumiwa na iliyotumiwa kwa niaba yake ya dhana, wasilisho la dhana, maandishi, picha, ujumbe, viungo, data, taarifa na nyenzo nyingine unazowasilisha (kwa pamoja, "Machapisho") kwenye Tovuti hii. Leseni hii haina vikwazo vya aina yoyote na bila malipo kwako kutoka kwa Tecno wala ruhusa au ilani, kwako au chombo kingine chochote. Leseni inajumuisha, haki ya kutengenea, kutumia, kuuza, kuzalisha tena, kuchapisha, kurekebisha, kulinganisha, kutayarisha kazi za utohozi, kuunganisha na kazi nyingine, kutafsiri, kusambaza, kuonyesha na kutoa leseni ndogo za Machapisho kwa njia, mfumo, au teknolojia inayojulikana sasa na itakayotengenezwa baadaye.

XI. Kanusho na Hakikisho

Tovuti, Maudhui na huduma zake zinatolewa “kama zilivyo” na “kama zinavyopatikana”. Tecno inakanusha moja kwa moja, kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria, hakikisho zote za aina yoyote, zilizoashiriwa au zilizopo, ikijumuisha lakini sio tu, hakikisho za uuzaji, uzima kwa ajili ya dhumuni fulani, umiliko, kutokiuka Haki za Mali ya Kiakili. Tecno haitoi hakikisho yoyote kwamba Tovuti haitatizwa, itakuwepo wakati wote, salama au bila hitilafu, au kasoro zozote zilizo kwenye Tovuti zitarekebishwa. Tecno haitoi hakikisho kwamba taarifa iliyo kwenye Tovuti au Maudhui ni sahihi au ni ya kuamini. Tecno haitoi hakikisho kwamba taarifa yoyote unayopakua kwenye Tovuti haitakuwa na virusi au bila kipengele kinachiweza kudhuru kiufundi. Tecno haitoi hakikisho kwa matendo, kutojumiishwa na matendo ya vyombo vyovyote vingine kuhisiana na utumizi wako wa Tovuti, Maudhui na huduma. Unapaswa kuwajibika kikamilifu kwa utumizi wako wa Tovuti na Maudhui. Suluhu yako pekee ya kutoridhika na Tovuti na maudhui yoyote ya Tecn ni kuacha kutumia Tovuti au maudhui hayo. Kipimo hiki cha suluhu ni sehemu ya maelewano kati ya wahusika wote wawili. Ikiwa Maudhui au huduma zitathibitishwa kuwa na kasoro, wewe na sio Tecno, utagharimia gharama zote za kufanya huduma na ukarabati.

XII. Kipimo cha Dhima

Kwa kiwango kimili kinachoruhusiwa na sheria, Tecno haitakuwa na dhima kwako au chombo kingine kinachodai kupitia wewe kwa harasa zozote zisizo za moja kwa moja, zisizo za kawaida, za kuigwa, za kiadhabu au zinazotokana na kitu kingine zinazoibuka kutokana au kuhusiana na wewe kuonyesha, kunakili au kupakua taarifa au nyenzo zilizo kwenye Tovuti, bila kujali kupoteza faida au manufaa mengine ya kiuchumi, hata ingawa Tecno imeshauriwa hapo awali kuhusu uwezekano wa hasara hizo.

Bila kujali Sheria, Tecno ikipatikana kuwa na dhima kwako kwa hasara au majeraha yoyote na yote yanayotokea wakati wa utumizi wako wa Tovuti au maudhui yoyote, kiwango cha juu zaidi ambacho Tecno itakufidia hakitakuwa zaidi ya kiwango jumla cha ada ulizolipa husiani na huduma yoyoye iliyo kwenye Tovuti kabla ya tarehe ya dai la kwanza uliloibua dhidi ya Tecno.

XIII. Uondoaji Lawama

Unakubali kutetea, kuondolea lawama na kuichukulia Tecno bila hatia, wakurugenzi, maofisa, washika dau, warithi, waajiriwa, mawakal, kampuni tanzu na washirika, wabia, waletaji na wanaoupa leseni kutoka na madai, hatua, hasara, dhima, gharama zote na zote, ikijumisha ada za wakili, ambazo zinakuwepo kufuatia ukiukaji wako wa Sheria, sheria husika na haki za Tecno na vyombo vingine, au kufuatia utuizi wako mbaya wa Tovuti au Maudhui, Uwasilishaji wa Mtumiaji, au huduma na shughuli zinazotokea wakati unatumia akaunti yako.

XIV. Usiri

Sera ya Faragha ya Tecno inatumika katika wakati wa kutumia Tovuti, masharti yake ni sehemu ya Sheria. Tafadhali pitia Sera ya Faraghaya Tovuti ambao imejumuishwa katika tovuti yetu. Tafadhali bonyeza hapa ili kutazama Sera yetu ya Usiri. Ikiwa haukubaliani na Sera hii ya Usiri, haijaidhinishwa kutumia Tovuti. Kando na hayo, kwa kutumia Tovuti hii, unakubali kwamba uwasilishaji wa Intaneti unaohusina na ufikiaji au utumiai wa Tovuti sio wa kibinafsi na salama. Pia unakubali kwamba ujumbe au taarifa yoyote unayotuma kwenye Tovuti inaweza kusomwa, kunakiliwa, kujazwa au kudakizwa na wengine, hata kama kuna ilani maalum kwamba uwasilishaji fulani umesimbwa na hauwezi kunakiliwa au kujazwa.

XV. Sheria Husika na Usuluhishaji Migogoro

Mgogoro, dai, tofauti au utata wowote mwingine unaoibuka kutokana au kuhusiana na ufikiaji au utumizi wako wa Tovuti na Sheria utatawaliwa, utakuwa chini na utatafsiriwa kulingana na sheria za Hong Kong, bila kuzingatia matukio ya ukinzani wa sheria husika. Mgogoro au tofauti yoyote kuhusiana na Sheria au Tovuti ambayo haiwezi kutatuliwa kikamilifu itatumwa na kusuluhishwa kikamilifu kwa suluhu inayotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Suluhu cha Hong Kong (HKIAC) chini ya Sheria za Suluhu Inayotolewa na Kituo cha Kimataifa cha Suluhu cha Hong Kong zinazotumika wakati Ilani ya Suluhu inapowasilishwa. Usuluhishaji utafanyikia Hong Kong. Lugha ya usuluhishaji itakuwa Kiingereza. Suluhu itakayotolewa itakuwa ya mwisho na itafuatwa na wahusika walio na mgogoro.

XVI. Ukiukaji Sheria

Ukikiuka Sheria, Tecno itakuwa na haki ya kusitisha, kuahirisha, au kubadilisha huduma unayopokea, au ufikiaji au utumizi wako wa sehemu ya Tovuti au yote, au kufunga au kufuta usajili wa akaunti yako uliyosajili na Tecno, bila sababu ya ziada, wakati wowote. Kando na hayo, Tecno inaweza kufichua taarifa zozote muhimu tuliyo nayo kukuhusu wewe ikiwa inahitajika au ni muhimu ili kushirikiana na mamlaka za utekelezaji sheria wakati wa kufunguliwa wakiukaji mashtaka. Unakiri kwamba utashirikiana na Tecno katika kuchunguza ukiukaji unaotuhumiwa na kwamba Tecno itakuwa na haki ya kufidiwa nawe ada za wakili na gharama za hatua hiyo, tukikuchukulia hatua ya kisheria kwa ajili ya ukiukaji wako wa Sheria hizi, pamoja na nafuu yoyote iliyokabidhdiwa Tecno. Pia unakubali kwamba ukiukaji wako wowote wa Sheria hizi utajumuisha mazoea haramu na yasio ya haki ya biashara, na utasababisha madhara mabaya kwa Tecno, kwa ambayo fidia za kifedha hazitatosha, na uko tayari kuipa Tecno nafuu sawia inayohitajika au iliyo mwafaka katika matuio hayo.

XVII. Haitumiki Mahali Ambapo Imepigwa Marufuku

Ingawa Tovuti hii inaweza kufikiwa kote ulimwenguni, si vipengele, bidhaa au huduma zote zilizojadiliwa, kurejelewa au zilizotolewa kupitia au kwenye Tovuti zinapatikana kwa watu wote au katika maeneo yote ya kijiografia. Tecno inahifadhi haki za kuweka kipimo, kwa hiarai yake pekee, cha utoaji na kiwango cha kipengele, bidhaa au huduma yoyote kwa mtu yeyote au eneo lolote la kijiografia. Utoaji wowote wa kipengele, bidhaa au huduma yoyote uliofanyika kwenye Tovuti hautumiki mahali ambapo umepigwa marufuku. Ukiamua kufikia Tovuti ukiwa nje ya eneo ambalo Tecno hufanyia kazi, unafanya hivyo kwa uamuzi wako binafsi na unawajibika peke yako katika kuambatana na sheria za eneo husika.

XVIII. Maoni

Unatambua kwamba maoni yako yoyote kuhusu kuimarisha Tovuti, bidhaa na/au huduma zozote za Tecno hazitachukuliwa kama taarifa ya faraghani. Hivyo basi, tunaruhusiwa kutumia taarifa hizo bila kipimo.

Hakimiliki © 2017 Tecno Inc. Haki zote zimehifadhiwa.